Bongo news
MATOKEO YA MITIHANI SASA KWANJIA YA SMS
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yanayotarajiwa kutoka mwezi huu, sasa yanaweza kupatikana kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia simu za mkononi.
Huduma hiyo ambayo ni mpya kuanza kutolewa hapa nchini na Afrika inajulikana kama ?Matokeo Chap Chap?.
Akizindua mpango huo mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya E-Life Group (T) Ltd, Bw. Benjamin Sitta, alisema mpango huo utamwezesha mwanafunzi kupata matokeo yake katika kipindi cha dakika moja.
Alisema mtu anayetaka kupata matokeo kupitia huduma hiyo anatakiwa kuandika herufi AX kwenye simu yake, namba ya kituo cha mtihani herufi X, namba ya mtahiniwa na kisha kutuma kwenye namba 15771.
Alisema mtu akitaka kujua alama alizopata anatakiwa kuandika herufi AX, namba ya kituo cha mtihani X namba ya mtahiniwa na kisha kutuma kwenda namba 15771.
?Utaratibu huu ni mwepesi sana, mfano AX S823X003 na kisha unatuma kwenda namba 15771 na hii ni ndani ya dakika moja unapata majibu yako,? alisema Bw.Sitta.
Alisema mpango huo tayari umeshaanza kufanyika kwenye shule za msingi.
Alisema katika mpango huo, wanafunzi ataweza kujua shule yake imekuwa ya ngapi kitaifa na mwanafunzi amekuwa wangapi kitaifa.
Aidha, alisema wahitimu wa kidato cha sita na ualimu wa daraja la kwanza pamoja na wale ya vyuo vikuu watapata matokeo yao kupitia mpango huo wa matokeo chap chap kwa njia ya simu zao za mikononi.
?Wanafunzi watakaotumia mpango huu wataweza kupata matokeo yao ndani ya dakika moja, unapokamilisa tu taratibu za kutuma ujumbe wako hata kabla haijapokelewa tayari unapata matokeo yako, ??alisema Bw.Sitta.
Alisema kwa miaka mingi watu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata matokeo yao na wamekuwa wakipata matokeo hayo baada ya zaidi ya wiki mbili tangu kutangazwa kwa matokeo hayo.
Mkurugenzi huyo alisema gharama zitakazokuwa zinatozwa kwa huduma hiyo ni Sh.500 kwa kila ujumbe.
Bw.Sitta alisema kwa kuanzia mpango huo utahusisha wateja wanaotumia mtandao wa Tigo na Celtel na kwa makampuni mengine ya Zantel na Vodacom wataweka huduma hiyo siku za karibuni.
?Tayari tumeshakamilisha huduma hii kwa wateja wa Tigo na Celtel lakini kwa wateja wa Voda na Zantel tuko kwenye hatua za mwisho kabisa ili nawao waweze kupata huduma hii ya matokeo chap chap,? alisema Bw.Sitta.
Kwa miaka mingi matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, cha sita na darasa la saba yamekuwa yakibandikwa katika mbao za ofisi za matangazo mashuleni na ofisi za elimu za wilaya na mikoa.
Mtihani wa taifa wa kidato cha nne ulifanyika mwezi Novemba mwaka jana.
There are no threads for this page.
Be the first to start a new thread.